Wakati wasanii
wakibongo kwa ujumla wao wakihangaika na shoo za Fiesta msimu huu,
Diamond ameendelea kujidhihilisha kwamba ni msaanii mkubwa sana kiasi
cha jamaa wa Clouds Entertainments kushidwa kumtumia vilivyo mwaka huu
kwenye show zao!
Ieleweke kwamba
kipindi hiki huwa ni cha neema kwa wasanii nyumbani ambao wengine
hufikia kuomba angalau tu wapate fursa japo tu ya kupanda jukwaani
kuonana na mashabiki.
Diamond kwa kipindi
kirefu sasa amekuwa ni msanii wa Tanzania mwenye show nyingi sana nje
ya nchi kiasi kwamba imeshindikana kumbakisha hapa nyumbani kushiriki
show za hapa.
Pamoja na upizani
mkubwa mno naoupata kijana ameendelea kukomaa na kujenga heshima hata
kwa wale ambao bado walikuwa wabishi kumkubali Diamond.
Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Tunachoweza kusema
kwa sasa ni kumtakia mafanikio mema na aendelee kufanya haya mapinduzi
makubwa kabisa kimuziki wa Tanzania. Keep it up Diamond.
Post a Comment