Chama
Cha Mapinduzi (CCM), kikiwa kimeweka bayana kwamba hakiungi mkono
Serikali tatu kama Rasimu ya Katiba inavyoonyesha, Waziri wa Katiba na
Sheria, Mathias Chikawe ameibuka na kusema endapo Mabaraza ya Katiba
yatawasilisha hoja za kuikubali, kuna uwezekano mkubwa wa Uchaguzi Mkuu
wa 2015 kukwama.Uwepo wa Serikali tatu
utafumua mfumo mzima wa utendaji ndani ya Serikali. Hatuwezi tena
kufanya uchaguzi wa Rais na wabunge 2015, hatuwezi kufanya chochote nje
ya Katiba ya Serikali Tatu kwa kuwa kinachofuata ni kuunda Katiba
nyingine inayohusiana na Serikali tatu.Kama
tutafanya uchaguzi, utafanyika kwa taratibu zipi, ipi itakuwa mipaka ya
marais wa Serikali tatu, makamu na mawaziri wakuu, mfumo wa Mahakama,
Tume ya Uchaguzi, utendaji wa Bunge na wabunge, yako mengi, sasa mpaka
hayo yaingie kwenye Katiba,” alisema Chikawe juzi Dar es Salaam.Alisema
lazima CCM isimamie suala hilo kwa kuwa kukubali Serikali tatu kutaua
Muungano ambao sehemu kubwa unalindwa na chama hicho tawala.“CCM
wamejipanga kama baraza na kusimamia hili la Serikali mbili ambalo
lengo ni kuulinda Muungano. Litakapokuja hili la Serikali tatu, lazima
Muungano uparaganyike,” alisema.Hata
hivyo, kauli hiyo ya Waziri Chikawe inakinzana na ile aliyoitoa Juni 4,
siku moja baada ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba kutangaza hadharani
Rasimu hiyo. NA MWANANCHI
Waziri
huyo alikaririwa na gazeti hili akisema upo uwezekazo wa Katiba Mpya ya
Tanzania Bara ikapatikana kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2015 ikiwa mchakato
wa Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano utakamilika kama inavyokusudiwa na
rasimu hiyo kupitishwa na wananchi katika ngazi zote bila mabadiliko.
“Watu
wasiwe na hofu. Sioni tatizo endapo rasimu itapita bila mabadiliko na
kupata Katiba Mpya. Aprili mwakani mpaka Desemba inatosha kabisa kuandaa
Katiba ya Tanzania Bara na tukaenda katika Uchaguzi Mkuu tukiwa na
Katiba Mpya,”alikaririwa akisema na kuongeza:
“Tunaweza
kuwatumia wajumbe walewale wa Tume ya Katiba lakini safari hii
tukawachukua wale wa Tanzania Bara pekee wakashiriki katika kuandaa
Katiba hiyo.”
Alisema
kutokana na muda kuwa mfupi, Tume hiyo inaweza isifanye kazi ya
kukusanya maoni kutoka kwa wananchi kama ilivyofanya sasa na badala yake
ikaandaa rasimu na kujadiliwa na wadau kisha kupelekwa katika mabaraza
ya Katiba kabla ya kupata Katiba Mpya.
Kwa
mujibu wa ratiba ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Katiba Mpya ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania inatarajiwa kukamilika Aprili mwakani.
Alisema
kuanzia hapo, Serikali inaweza kuitumia tume ya sasa kutangaza rasimu ya
kwanza ya Katiba ya Tanzania Bara kwa kurejea maoni iliyokusanya hivyo
hatua ya kwanza ikawa ni kujadiliwa kwa rasimu hiyo kwenye mabaraza ya
Katiba kwa miezi miwili na baadaye kupelekwa katika Bunge la Katiba
jambo litakaloifanya ipatikane mapema.
Post a Comment