Tatizo la usalama wa waandishi wa habari nchini, lilikuwa ndiyo ajenda kuu katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, yaliyofanyika kwa siku mbili mjini Arusha, yakiwakusanya wanahabari kutoka nchi za Afrika Mashariki.
VITENDO vya hivi karibuni vya mauaji na utesaji wa waandishi wa habari nchini, vimechafua jina la Tanzania baada ya taarifa hizo kusambaa katika nchi mbalimbali duniani.
Tatizo la usalama wa waandishi wa habari
nchini, lilikuwa ndiyo ajenda kuu katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru
wa Vyombo vya Habari Duniani, yaliyofanyika kwa siku mbili mjini Arusha,
yakiwakusanya wanahabari kutoka nchi za Afrika Mashariki.
Maadhimisho hayo ya Mei 3 na 4 mwaka
huu, yalizinduliwa kwa machapisho kadhaa likiwamo toleo la 19 liitwalo
“So this is democracy?” (Kwa hiyo hii ndiyo demokrasia?), lilitolewa na
Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (Misa).
Kitabu hicho ambacho ni zao la nchi za
Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), kinaitaja Tanzania kwamba
ni kinara wa vitendo vya kuteka, kushambulia na kuuawa kwa waandishi wa
habari na wanaharakati katika kipindi cha mwaka jana na miezi ya mwanzo
ya mwaka huu.
Tukio la mauaji ya aliyekuwa mwandishi
wa habari wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Daudi Mwangosi
linatajwa kuwa moja ya matukio mabaya dhidi ya uhuru wa habari
yaliyotokea mwaka jana katika Ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika.
Jalada la nje na ukurasa wa kwanza wa
kitabu hicho imepambwa na picha ya askari polisi wanaomshambulia
marehemu Mwangosi kwa kipigo, muda mfupi kabla ya kulipu
liwa kwa bomu la kishindo la kutoa machozi ambalo lilisambaratisha baadhi ya viungo vyake na hatimaye, kifo chake.
Kitabu hicho cha kurasa 258 pia
kimetumia maelezo ya awali kutaja tukio la kushambuliwa kwa Mwenyekiti
wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Absalom Kibanda kama mifano ya matukio
mabaya yaliyowakumba waandishi wa habari nchini.
Katika utangulizi wa kitabu hicho,
Mkurugenzi wa Kanda wa Misa-Tan, Zoe Titus ametoa mifano ya matukio ya
Tanzania kwamba ni uthibitisho kwamba taasisi yake ilifanya makosa
katika miaka ya nyuma kutoa taarifa zinazoeleza kwamba matukio ya
kushambuliwa kwa waandishi wa habari yamekuwa yakipungua.
“Mwaka 2012 umekuwa mwaka wenye
changamoto kubwa kutokana na kurejea kwa matukio ya kushambuliwa kwa
waandishi wa habari, tunaweza kusema tulifanya makosa kusema kwamba
mashambulizi dhidi ya waandishi wa habari yanapungua katika nchi zetu,”
anasema Titus katika maelezo yake.
Maelezo mengine kuhusu Tanzania
yanapatikana kuanzia ukurasa wa 144 hadi 150 ambapo hali halisi ya uhuru
wa habari, kukusanyika na kujieleza imezungumziwa, huku sheria mbaya
ikiwemo ile ya magazeti ya mwaka 1976 zikitajwa kama vikwazo.
Mashtaka ya jinai kwa makosa
yanayotokana na habari zinazochapishwa au kutangazwa kwenye vyombo vya
habari ikiwemo ile inayomkabili Kibanda na aliyekuwa Kaimu Mtendaji Mkuu
wa Mwananchi Communications Ltd, Theophil Makunga, ni miongoni mwa
vikwazo kwa uhuru wa habari na kujieleza vinavyotajwa kwenye kitabu
hicho.
Kifo chenye utata cha mwandishi wa Kituo
cha Redio Kwezira cha Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma, Issa Ngumba na
lile la kujeruhiwa kwa kupigwa risasi kwa mwandishi Shaban Matutu wa
gazeti la Tanzania Daima, pia yametajwa na kuhusishwa na kazi zao ingawa
hadi sasa haijathibitika.
Chanzo cha Habari: Mwananchi
Post a Comment