Habari,
Leo naomba niwatangazie wadau wangu na
mashabiki wote waliokuwa wakinipenda kipindi nikiwa nawadj wasanii wa
hapa nchini na hata wale wasanii waliokuwa wakitoka nje ya bongo.
Natangaza rasmi kupumzika kazi hii ya uDJ niliyoanza nayo toka 2005
mpaka leo, sababu za kupumzika nimeona nipumzishe uDJ niendelee na kazi
inayoniingizia kipato nazungumzia website yangu hii tokea ikiwa ni blog.
Kazi ya kudj wasanii ni kazi fulani nzuri
lakini ni ngumu sana usipokuwa na hobby nayo, nimeifanya kazi hii kwa
mapenzi yangu mwenyewe yakupenda mziki na sikuwahi kulalamika mslahi
ninayoyapata kwasababu niliifanya kazi hii kwa mapenzi yangu mwenyewe
hata napokuwa jukwaani nilikuwa nafurahia sana. Lakini kwa kuwa kazi hii
ya kuandika habari na kuonyesha kazi za wasanii wa hapa nchini ndio
inayonilipa vizuri basi naona sina budi kupumzisha kimoja ili niendelee
na kimoja.
Baada ya kupumzisha kazi yakudj kwenye
majukwaa na kuwadj wasanii sasa nitakuwa naendelea na kazi yakuvumbua
vipaji vya wasanii pia nitaendelee na mix tape zangu kama kawaida.
Msanii atakayenihitaji sasa hivi basi ujue itakuwa kazi yakwenda kupiga
picha show zake au kurecord show zake TU akiwa jukwaani. Mbali na hapo
nitaendelea kupromoti mziki wa nyumbani na wasanii wake mpaka mwisho
wangu. Nawakaribisha madj wadogo ambao mlipenda kuwa madj wa wasanii na
hamkujua jinsi yakuanzia, nitawashauri na pia nitawafundisha njia za
kuwadj wasanii hususani wasanii wa Hip Hop na Bongo Fleva unacheza nao
vipi unapokuwa nao jukwaani.
Nawapenda sana wadau wote wa DJCHOKA MUSIC kwasababu bila nyie hakuna mimi
ONE
DJ CHOKA
Post a Comment