0

Moses Kulola, niliyezaliwa 1928 katika familia ya watoto kumi, ambapo watano  tuko hai hadi sasa, nilijiandikisha katika shule yangu ya kwanza mnamo mwaka 1939. Shule hiyo ilikuwa inaitwa Ligsha Sukuma, ikiwa ni shule ya Misheni. Baada ya kumaliza hapo Ligsha Sukuma Mission School nikajiunga katika Idara ya  Uchoraji wa Majengo mnamo mwaka 1949. Na mwaka 1950 nikabatizwa katika Kanisa la AIM Makongoro, mjini Mwanza..

Nimemuoa Elizabeth na Mungu alitujalia kupata watoto 10, ambapo kwa sasa saba (7) bado wako hai.  Nilianza kazi za Umisionari mnamo mwaka 1950, ingawa nilikuwa nimesikia wito huo mwaka ule wa 1949!

Mwaka 1959 niliajiriwa serikalini. Lakini pamoja na kuajiriwa huko mimi niliendelea na kuhubiri Injili katika Miji na Vijiji. Utumishi wangu kama mwajiriwa wa Serikali ulikwisha mwaka 1962 baada ya kuwa nimekabidhi nguvu, mwili na nafsi yangu katika kazi ya Mungu! Ilipofika mwaka 1964 niliamua kusoma na nikajiunga katika  Chuo cha Theolojia na kuhitimu katika kiwango cha Diploma mnamo mwaka ule wa 1966.

Baada kupata Diploma hiyo sikuishia hapo bali niliendelea kusoma kwa Njia ya Posta na kupata Vyeti vingi sana kutoka Sehemu mbali mbali duniani.

Nilitumika miaka miwili kama mchungaji, 1961-1962, katika kanisa hilo la AIM na baada ya hapo nikawa muumini wa Kipentekoste. Halafu nikatumika katika kanisa la TACR kuanzia 1966 hadi 1991 ambapo nilijisikia kuanzisha Evangelistic Assemblie of God, maarufu kama EAGT. EAGT ni kanisa ambalo limefanikiwa kukua kwa kasi kubwa nchini hasaTanzania, Zambia naMalawi ambapo jumla yake ni kama makanisa 4,000 yakiwa ni makanisa makubwa na madogo, na mimi Moses Kulola nikiwa ndiye Askofu Mkuu na Msaidi wangu akiwa Askofu Mwaisabira.

Faustine Munishi(malebo) Moses Kulola,Emmanuel Mwasota.

Si kazi rahisi kuendesha makanisa elfu nne (4,000) na ndiyo maana ilibidi kugawanya katika maeneo 34 ya kiutendaji, kukiwa na Kanda Tano ili kurahisisha kazi hiyo ya Mungu. Kila eneo na Kanda kuna mwangalizi wake.

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Top