0
Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva (kushoto) akijikunja kupiga shuti huku beki wa Coastal, Juma Nyoso, akijaribu kumdhibiti, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom unaoendelea hivi sasa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Na Waandishi Wetu. LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, imeendelea leo katika viwanja tofauti na mabingwa watetezi, Yanga SC wamelazimishwa sare ya 1-1 na Coastal Union, huku Simba SC wakiibwaga JKT Oljoro 1-0 mjini Arusha wakati Azam FC wakiitandika bao 2-0 Rhino Rangers ya Tabora.

Tabora:
Hadi mapumziko hakukuwa na timu iliyopata bao na kipindi cha pili, iliwachukua dakika 11 tu Azam kup
ata bao la kwanza lililofugnwa na Mwaikimba.


Mwaikimba alifunga bao hilo dakika ya 56, baada ya kupokea pasi ya kutanguliziwa pembeni kulia na Salum Abubakar ‘Sure Boy’, kisha akamtoka beki wa Rhino, Hussein Msabila na kuingia ndani kidogo na kipa Abdulkarim Mtumwa akavutika, hivyo kumpa kazi rahisi mshambuliaji wa Azam kukwamisha mpira nyavuni.    

Seif aliyeingia kipindi cha pili, alifunga bao la pili dakika ya 78 kwa pasi ya Himid Mao Mkami aliyeingia pia kipindi cha pili. 

Mchezo ulikuwa mkali na wa nguvu jambo ambalo lilimfanya mfungaji bora wa Ligi Kuu, Kipre Tchetche acheze kwa dakika 28 tu baada ya kuumia mguu wa kulia kufuatia kukanyagwa na beki wa Rhino, Laban Kambole. 

Kikosi cha Rhino kilikuwa; Abdulkarim Mtumwa, Ally Ahmed, Hussein Msabila, Julius Masunga, Laban Kambole, Stanslaus Mwakitosi, Shiya Sanja, Emma Yasile, Victor Hangaya, Nurdin Bakari/Daniel Manyanya dk 85 na Shija Makula/Msafiri Abdallah dk31.

Azam FC; Mwadini Ally, Erasto Nyoni, Waziri Salum, Aggrey Morris, Joackins Atudo, Kipre Balou, Jabir Aziz, Khamis Mcha ‘Vialli’/Himid Mao dk75, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Gaudence Mwaikimba na Kipre Tchetche/Seif Abdallah dk30. 
  Dar es Salaam; Yanga SC ilitangulia kupata bao dakika ya 65 mfungaji Mrundi Didier Kavumbangu na Coastal ikasawazisha kwa penalti dakika ya 90 kupitia kwa Mkenya Jerry Santo.

Lakini sifa zimuendee kiungo Haruna Moshi ‘Boban’ ambaye alimnawisha mpira beki mmoja wa Yanga na kuzaa penalti hiyo. Dakika ya 77, Crispin Odula na Simon Msuva wote walitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kugombana.

Yanga SC; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, David Luhende, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Mbuyu Twite, Salum Telela/Hamisi Thabit dk46, Simon Msuva, Frank Domayo, Didier Kavumbangu, Jerry Tegete/Hussein Javu dk46 na Haruna Niyonzima.

Coastal; Shaaban Kado, Juma Hamad, Abdi Banda, Marcus Ndehela, Juma Nyosso, Jerry Santo, Uhuru Suleiman/Suleiman Kassim ‘Selembe’ dk43, Crispine Odula, Yayo Lutimba, Haruna Moshi na Danny Lyanga/Kenneth Masumbuko dk62.

Arusha; Bao pekee la Haruna Othman Chanongo dakika ya 34, leo limeipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji JKT Oljoro kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Chanongo alifunga bao hilo kwa shuti la mbali dakika ya 34 na kuwainua vitini wapenzi wa Simba SC, ambao katika mechi ya kwanza walinuna baada ya timu yao kulazimishwa sare ya 2-2 na Rhino mjini Tabora.

Simba SC; Abbel Dhaira, Nassor Masoud ‘Chollo’, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Gilbert Kaze, Joseph Owino, Jonas Mkude, Amri Kiemba, Abdulhalim Humud, Betram Mombeki Tambwe Amisi na Haroun Chanongo.  

JKT Oljoro; Shaibu Issa, Yussuf Machogote, Napho Zuberi, Nurdin Mohamed, Shaibu Nayopa, Babu Ally, Salleh Iddi, Hamisi Saleh, Amir Omar, Sabri Ally na Essau Sanu. 

Morogoro; Bao pekee la Masoud Ally dakika ya 73, liliipa Mtibwa Sugar ushindi wa 1-0 dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani mjini Morogoro.

Mbeya; Wenyeji Mbeya City wameshinda 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya. Mabao ya wenyeji yalifungwa na Paul Nonga dakika ya saba na Steven Mazanda dakika ya 90, wakati bao la Ruvu lilifungwa na Shaaban Suzan dakika ya 24. 

Tanga; Bao pekee la Fully Maganga dakika ya 62, lilitosha kuipa Mgambo JKT ushindi wa 1-0 dhidi ya Ashanti United kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Chamazi; Kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Dar es Salaam, JKT Ruvu iliendeleza wimbi la ushindi baada ya kuilaza Prisons 3-0. Mabao ya JKT yalifungwa na Machaku Salum dakika ya 44, Emmanuel Swita dakika ya 69 na Hussein Bunu dakika ya 87

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
Top