Kwa
mara ya kwanza muigizaji wa filamu, Elizabeth Michael aka Lulu jana
alifanya interview ya kwanza tangu atoke gerezani January mwaka huu.
Lulu
aliye na muonekano wa ‘udada’ zaidi alihojiwa jana kwenye kipindi cha
Take One cha Clouds TV kinachoendeshwa na Zamaradi Mketema.
Katia
interview hiyo, Lulu aliongea masuala mengi kuhusu maisha yake ya sasa,
mipango yake na mengine lakini akidai kuwa hatopenda kuongelea suala la
uhusiano wake na Kanumba kwakuwa anahisi bado hajawa tayari ila muda
ukifika atafunguka mengi. Haya ni baadhi ya masuala aliyoyazungumza.
Kuhusu uzinduzi wa filamu yake mpya Foolish Age
Nitahitaji
watu waone baadhi ya vitu vilivyopo kwenye movie. Movie inaitwa Foolish
Age. Nitaizindua chini ya kampuni ya Proen (????) Promotions Ltd na ni
kampuni ambayo ndio inanimanage kwa sasa.
Kuhusu kama ana boyfriend aliyemnunulia vitu vya thamani
Watanzania
wengi tulishajiwekea ile dhana kwamba ‘ukiona mwanamke amefanya kitu
basi there is a man behind, yaani ni ile dhani ipo tayari ndani yetu
kwahiyo hata kama mtu atastruggle kutafuta kitu chake mwenyewe lakini
hiyo itakuwa ni ukweli wako na unaujua mwenyewe .
Kiukweli
ni kwamba hakuna mwanaume yeyote ambaye amenifanyia chochote till now.
Nachoshukuru tu ni menejimenti yangu, kampuni ambayo nafanya nayo kazi.
Ni
kampuni ambayo inanijali, inajali kazi zangu, inajali msanii wao
kwahiyo whatever I’m having, whatever I’m doing ni mimi mwenyewe, ni
kazi zangu ni biashara yangu.
Uhusiano wake na Mama Kanumba na jinsi alivyompata kufanya naye movie ‘Mapenzi ya Mungu’
Kwa
sasa hivi tupo kama familia kwa hiyo it wasn’t hard mimi kumpata na
nilijisikia vizuri kama ntaweza kufanya naye kazi. Kuna spirit ambayo
ilinivuta zaidi nifanya kazi na Mama Kanumba kuliko labda mama mwingine.
Anachomiss kwa Kanumba
Busara zake, he was a person ambaye akikuona unaenda hivi he takes you in the right way.
Kuhusu kwanini mapenzi yake na Kanumba yalikuwa siri
Ni makubaliano tu and there was no need like to let people know yaani kumfanya kila mtu ajue nadhani haikuwa na maana kwetu.
Kuhusu kwanini alinenepa alipokuwa gerezani
Labda
kwasababu nilimwachia Mungu kila kitu, nilimkabidhi Mungu kila kitu so I
had this peace of mind. Niliacha kwamba yeye ni msimamizi wa kila kitu.
Let me confess kwamba gerezani kumenifanya nimjue Mungu vizuri sana,.
Kumenifanya
nimjue na nimwamini na kumjua na kumwamini kumetokana kwamba kuna vitu
vingi vimekuwa vinafanyika like naviona hivi kwa macho na naona kabisa
kwamba hapa ingekuwa mimi kama mimi ama binadamu yeyote haiwezekani...
So ni Mungu tu ndio ameweza kufanya hili likapita. Kwahiyo niliamua tu kumwachia yeye kila kitu nikajikuta tu nina amani.
Post a Comment