Chama Cha Wananchi (CUF), kimesema maandamano ambayo awali kilipanga kufanya Juni 29, mwaka huu kuelekea Ikulu lakini yakaahirishwa kutokana na ziara ya Rais wa Marekani, Barack Obama yako pale pale.
Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara, Julius Mtatiro, alisema kwa sasa viongozi wengi wa chama wapo mikoani, lakini watakaporudi jijini Dar es Salaam chama kitafan
ya mkutano utakaopanga lini maandamano hayo yafanyike.
“Hatujakutana bado. Wajumbe wengi tupo mikoani. Sasa tutakaporejea Dar es Salaam tutapanga siku ya kukutana. Halafu tutapanga siku ya maandamano na tutawajulisha,” alisema Mtatiro.
Kwa mujibu wa CUF, maandamano hayo yana lengo la kumfikishia ujumbe Rais Jakaya Kikwete, kwa kile wanachodai kuwa vitendo vya ukatili, wizi, ubakaji na mauaji vinavyofanywa na polisi mkoani Mtwara na kutaka uchunguzi kuhusu matukio ya Arusha.
Hata hivyo, kuahirishwa kwa maandamano hayo kulikuja baada ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, kuyapiga marufuku na kuonya kwamba polisi wangepambana na yeyote ambaye angekaidi amri hiyo.
SOURCE:
NIPASHE
Post a Comment