BASI LA KAMPUNI YA SAIBABA LIKIWA LIMEACHA NJIA
WATU 21
wamejeruhiwa vibaya na wengine 30 wakinusurika kifo baada ya basi
walilokuwa wakisafiria kutoka jijini Dar es salaam kwenda Songea kupata
ajali eneo la vigwaza mkoani Pwani.
akizungumza
na MCHOME BLOG mkuu wa kikosi cha askari wa barabarani Chalinze
Assistance Inspector Sule amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa
mbili asubuhi ya leo July 02 baada ya basi la abiria la kampuni ya
Saibaba lenye namba za usajili T 779 BKL kutaka kulipita gari lingine
huku likiwa katika mwendo kasi na hatimaye gari lilimshinda dereva huyo
na kisha kupinduka.
Aidha
ameongeza kuwa majeruhi hao wamekimbizwa katika hosiptali ya tumbi
kibaha kwaajili ya matibabu, basi hilo lilikuwa na jumla ya abiria 51.
Habari kwa hisani ya www.mchomeblog.co
Post a Comment